WAKATI mtandao huu ukipiga picha hizi pale Mango Garden Kinondoni Machi 27 mwaka huu, Saluti5 haikujua kama ndio ilikuwa inampiga picha kwa mara ya mwisho mwigizaji nyota Adam Kuambiana.
Adam Kuambiana alifariki ghafla jana asubuhi na kufanya picha hizi zilizopigwa kwenye onyesho la Mashauzi Classic ziwe ndio picha zake za mwisho kuingia kwenye maktaba ya Saluti5.
Inawezekana kabisa kuwa hata watu waliopiga picha hizi na Adam Kuambiana, pengine ndio picha zao za mwisho kupiga nae.
Hebu zitupie macho picha hizi pengine zinaweza zikakukumbusha kitu kuhusu safari ya binaadamu. Hakika kifo hakina hodi.
Hapa ni Isha Mashauzi akiwa na Adam Kuambiana
Adam Kuambiana na Isha
Hapa Adam Kuambiana akiwa na Said Mdoe (kushoto)
Isha Mashauzi na Adam Kuambiana
Isha Mashauzi, Adam Kuambiana, Said Mdoe
Adam Kuambiana na Banana Zorro
Adam Kuambiana na Banana Zorro
Adam Kuambiana na Banana Zorro
No comments:
Post a Comment