May 19, 2014

MWILI WA ADAM KUAMBIANA KULALA BUNJU JUMATATU … JUMANNE ASUBUHI UNAPELEKWA LEADERS CLUB

 
 
 
 
MWILI WA ADAM KUAMBIANA KULALA BUNJU JUMATATU … JUMANNE ASUBUHI UNAPELEKWA LEADERS CLUB

MWILI wa mwongozaji na mwigizaji wa filamu za kibongo, Adam Kuambiana (pichani), aliyefariki Jana asubuhi, kesho Jumatatu utapelekwa Bunju nyumbani kwa mkewe kwaajili ya kuagwa.

Kwa mujibu wa Rais wa Bongo Movie Unit, Steve Nyerere, mwili wa Adam utalazwa hapo kabla ya Jumanne asubuhi kupelekwa Leaders Club Kinondoni ambapo heshima za mwisho zitatolewa hadi mchana na kisha utakwenda kuhifadhiwa kwenye makazi yake ya milele makaburi ya Kinondoni.

Kwa sasa mwili wa Adam Kuambiana bado upo chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Muhimbili.

No comments:

Post a Comment