May 18, 2014

MAJANGA: FILAMU YA ZENA NA BETINA YAMTIA MATATANI MWANADADA NISHA,, ATOZWA FAINI MILIONI 100 NA GAZETI LA SANI

 
 
 
 
Zikiwa zimesalia siku kumi na mbili Zena NA Betina kulitikisa soko la filamu Bongo 
MWANADADA Salma Jabu Nisha akizungumza na Website hii ya thechoicetz asubuhi ya leo alizungumzia suala la kuchimbwa mkwara mzito na Gazeti La Sani kwa kuambiwa alipe fedha taslimu za kitanzania Shilingi milioni 100 iwapo 
anataka kuendelea kuyatumia majina hayo ya Zena NA Betina au laa sivyo atashtakiwa na Gazeti hilo.  


Nisha alisema: Jamani navyoelewa katika sheria ya jamhuri ya muungano watanzania ya mwaka 1971ibara ya pili kifungu 'A' kuhusu matumizi ya majina ina sema kila mtu anahaki ya kutumia jina lolote alipendalo mradi awe amepewa na wazazi au kurithi,  
Majina hayo ni ,A' MAJINA YA ASILI, mfano Mwajuma, Amina,Zena, Hamis, Kabuti n.k, Kupitia sheria hii ndio maana unakuta majina hufanana.. 
 
 Swali je wenye majina yao kweli hao wa kina zena wakiamua washtaki gazeti la sani kwa kuwafananisha na katuni wanaweza kuwalipa zena wote Tanzania?....Hakuwa na mengi ya kusema Nisha bebe bali alimalizia kwa kusema kuwa mashabiki wake wakae mkao wakula ZENA na BETINA zimesalia siku kumi na mbili iwasili madukani kote.
 Salma Jabu Nisha

No comments:

Post a Comment