October 15, 2015

MPIGA PICHA NA FAMILIA YAKE WAUAWA BURUNDI


MPIGA PICHA NA FAMILIA YAKE WAUAWA BURUNDI
Image copyrightGetty
Image captionMaafisa wa polisi Burundi
Mpiga picha wa runinga ya taifa nchini Burundi, pamoja na familia yake wameuawa katika mji mkuu Bujumbura.


Polisi mjini humo wanasema kuwa walikuwa wakijaribu kuwaokoa maafisa wenzao wa polisi waliokuwa wametekwa nyara.
Polisi wanasema kuwa watu kumi waliuawa katika kisa hicho akiwemo mpiga picha huyo wa runinga Christophe Nkeza-bahizi, mkewe na wanawe wawili pamoja na afisa mmoja wa polisi.
Image captionWaziri wa usalama nchini humo Bunyoni
Milio ya risasi na na milipuko ya mabomu yalisikika usiku kucha.
Ghasia nchini Burundi, zilianza mwezi Aprili mwaka huu, baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza angewania muhula wa tatu wa urais.
Katika miezi ya hivi karibuni, Burundi imekumbwa na wimbi la mauaji ya kiholela ya wanaharakati wa upinzani na maafisa wa usalama.
Haijajulikana mara moja ni nani aliyewateka nyara maafisa hao wa polisi.


No comments:

Post a Comment