June 26, 2014

UFARANSA, USWISI ZAPETA HATUA YA 16 KOMBE LA DUNIA,

 
TIMU ya Taifa ya Ufaransa imefuzu hatua ya 16 ya kombe la dunia kama washindi wa kwanza wa kundi E baada ya usiku huu kuambulia pointi moja kufutia suluhu ya bila kufungana na Ecuador.
Ufaransa wamefikisha pointi 7 kileleni wakifuatiwa na Uswisi wenye pointi 6 katika nafasi ya pili baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Honduras.
 
Mabao yote ya Uswisi yamefungwa na Xherdan Shaqiri katika dakika ya 5, 30 na 70.Kwa matokeo hayo, Ecuador waliomaliza katika nafasi ya nne kwa pointi 4 na Honduras walioshika mkia bila pointi yoyote wameaga rasmi mashindano ya mwaka huu ya kombe la dunia.
 
Kikosi cha Ecuador: Dominguez, Paredes, Guagua, Erazo, Walter Ayovi, Antonio Valencia, Minda, Noboa (Caicedo 89), Montero (Ibarra 63), Arroyo (Achilier 82), Enner Valencia.
Wachezaji wa akiba: Banguera, Mendez, Rojas, Jaime Ayovi, Bagui, Saritama, Martinez, Gruezo, Bone.
Kadi ya njano: Erazo.
Kadi nyekundu: Antonio Valencia.
Kikosi cha Ufaransa: Lloris, Sagna, Koscielny, Sakho (Varane 61), Digne, Griezmann (Remy 79), Pogba, Schneiderlin, Matuidi (Giroud 67), Sissoko, Benzema.
Wachezaji wa akiba: Ruffier, Debuchy, Evra, Cabaye, Cabella, Valbuena, Mavuba, Mangala, Landreau.
Mwamuzi: Noumandiez Doue (Ivory Coast)
Kikosi cha Honduras: Valladares, Figueroa, Bernardez, J Garcia, W Palacios, Bengtson, Costly, B Garcia, Espinoza, Claros, Beckeles.
Kikosi cha Switzerland: Benaglio, Lichtsteiner, Inler, Xhaka, Behrami, Rodriguez, Mehmedi, Drmic, Djourou, Schaer, Shaqiri.
 

No comments:

Post a Comment