June 02, 2014

MAONESHO YA BIDHAA ZA TANZANIA KATIKA UBALOZI WA TANZANIA LUSAKA, ZAMBIA (TANZANIA WEEK) KUANZA 25 -31 JULAI 2014



MAONESHO YA BIDHAA ZA TANZANIA KATIKA UBALOZI WA TANZANIA LUSAKA, ZAMBIA (TANZANIA WEEK) KUANZA 25 -31 JULAI 2014
Katika kuendelea kusherehekea Muungano wetu na pia kujiunga na wenzetu wa nchi ya Zambia ambao nao mwaka huu wanasherehekea miaka 50 tangu wapate Uhuru (25 Oktoba), Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia unapenda kuwajulisha kuwa umeandaa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania.

Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia unachukua nafasi hii kuwakaribisha rasmi Watanzania kuja kushiriki katika maonesho haya. Tuna amini ni nafasi nzuri ya kujitanganza na kuonana uso kwa uso na wadau mbalimbali ili kupanua wigo wa biashara.
Maonesho haya ambayo yamebeba jina la "TANZANIA WEEK" yatafanyika katika viwanja vya Ofisi ya Ubalozi Lusaka, Zambia, kuanzia tarehe 25 hadi 31 Julai 2014.

Kwa maelezo zaidi na mawasiliano tumia njia zifuatazo:

     Nukushi ya Ubalozi: tanzanhighcom@zambia.co.zm
     Namba ya Simu: +260211253323/4 
     
Maafisa wa Ubalozi;
      
i) Bibi Justa M. Nyange - simu ya kiganjani +260-979-401-433 
      Nukushi : kitutuj@yahoo.com

    ii) Bw. Richard M. Lupembe  - simu ya kiganjani +260-965-031-754
          Nukushi : rlupembe@yahoo.com.

    iii) Bw. Mogosi S. Munatta - simu ya kiganjani +260-979-411-011
          Nukushi : munatta@yahoo.co.in.
      
   iv)  Bw. Huddy A. Kiangi …….simu ya kiganjani +260-977-934-240
         Nukushi : hkiangi@yahoo.com.


KARIBU SANA LUSAKA, ZAMBIA


No comments:

Post a Comment