June 11, 2014

MAJANGA KWA KOCHA WA BRAZIL LUIZ FELIPE SCOLARI, BINAMU YAKE AFARIKI KWENYE AJALI YA GARI ...hatarini kukosa mechi ya ufunguzi



MAJANGA KWA KOCHA WA BRAZIL LUIZ FELIPE SCOLARI, BINAMU YAKE AFARIKI KWENYE AJALI YA GARI ...hatarini kukosa mechi ya ufunguzi

In charge: Luiz Felipe Scolari is preparing his team                for Brazil's World Cup opener against Croatia

KOCHA wa Brazil Luiz Felipe Scolari huenda akaondoka kwa muda kwenye kambi ya timu yake baada ya mpwa wake kufariki kwenye ajali ya gari.

Scolari, ambaye kikosi chake kitaumana na Croatia kwenye mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia siku ya Alhamisi, aliwahi kuondoka tena kwenye kambi hiyo mwezi uliopita pale alipoenda kuhudhuria mazishi ya shemeji yake.

Binamu yake ambaye ni mfanyabiashara aliyetajwa kwa jina la Tarcisio Joao Schneider, alikufa baada ya gari lake kugongana na gari kubwa kusini mwa Rio Grande do Sul.

Msemaji wa polisi aliiambia Reuters kuwa Schneider alikuwa peke yake kwenye gari. Dereva wa gari kubwa hakupata majeraha yoyote.



No comments:

Post a Comment