Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akitoa heshima za
mwishomapema katika viwanja vya Leaders kwa mwili wa msanii wa Filamu nchini
Marehemu Adam Philip Kuambiana aliyefariki ghafla mwishoni mwa wiki jijini Dar
es Salaam.
Mjane
wa marehemu Adam Kuambiana, Bi. Janeth Rite akiwa katika wakati mgumu kutokana
na kushuhudia mwili wa mme wake ukiwa katika
jeneza.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akitoa salamu za
rambirambi kwa niaba ya Serikali, kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa
marehemu Adam Philip Kuambiana wakati wa shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa
marehemu iliyofanyika leo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam,
kushoto ni mjane wa marehemu Bi. Janeth Rite.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisso akitoa salamu za
rambirambi kwa niaba ya Bodi ya Filamu kwa familia ya marehemu Adamu
PhilipKuambiana aliyekuwa msanii wa Filamu na mkurugenzi wa Kampuni ya
kutengeneza filamu ya APK akiyefariki ghafla siku ya jumamosi kutokana na
ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akitoa salaam za rambirambi kwa
niaba ya Manispaa ya Kinondoni ambapo mjane wa marehemu Adam Kuambiana
anafanyakazi kama Diwani wa Kata ya Kunduchi. ,kushoto katikati ni Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara na mjane wa marehemu
Mhe. Janeth Rite
Msanii
wa Muziki wa injili na Bongo Flava Stara Thomas akiimba kwa hisia wakati wa
shughuli ya kutoa heshi za mwisho kwa mwili wa marehemu Adam Kuambiana leo
katika viwanja vya leaders jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bongo Movie Steve Mengere maarufu kama Steve Nyerere akitoa salaam za
rambirambi kwa niaba ya Bongo Movie wakati wa shughuli za kutoa heshima za
mwisho kwa mwili wa marehemu Adam Philip Kuambiana.
Msanii
wa Filamu Jacob Steven – JB akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa marehemu Adam
Kuambiana katika tasnia ya Filamu nchini,katika maelezo yake JB amesema kuwa
Adam alikuwa injini katika sanaa ya filamu hivyo ni pengo kubwa ambalo hajui
litazibika namna gani.
Msanii
wa Filamu nchini Wema Isack Sepetu akiwa katika majonzi makubwa wakati wa
shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa msanii mwenzake marehemu Adam
Philip Kuambiana iliyofanyika katika viwanja vya Leaders jana jijini Dar es
Salaam.

Baadhi
ya wananchi waliohudhuria shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa
marehemu Adam Kuambiana wakiwa katika taswira mbalimbali.
Picha
zote na Frank Shija, Afisa Mawasiliano
Serikalini-WHVUM
No comments:
Post a Comment