May 21, 2014

Tumepata Tenda ha ha ha ha ha

Blogu imepata tenda toka shirika la kimataifa kufanya utafiti ufuatao (tafadhali kama una jibu tusaidie tupate mkwanja):
• Nchi gani ambapo wadada hawataki kupewa maua siku za Valentine na bethde zao?
• Wapi ambako wazazi wote kila moja anadai alikuwaga wa kwanza darasani?
• Wapi ambako unaweza kuwa na leseni ya udereva wakati hujawahi kushika usukani hata siku moja?
• Wapi ambapo viongozi wa serikali hawajui kuimba wimbo wa Taifa?
• Wapi ambapo wananchi wanaweza kukuua kwa kuiba kuku na wakakuabudu kwa kuiba mabilioni?
• Wapi ambapo watu hugombania kuingia darasani, mpirani na hata kwenye mabasi?
• Wapi ambapo kila unaekutana nae amewahi kuibiwa simu?
• Wapi ambapo unaruhusiwa kulalamika kuwa ndugu zako wamekuroga kwa kila tatizo?
• Wapi ambapo matajiri wote wana vitambi?
• Wapi ambapo iPhone 5 zinauzwa kwenye foleni za magari kwa shilingi laki moja?
• Wapi ambapo kupata dhamani polisi lazima ulipie?
• Wapi ambapo basi la watu 25 linaweza kubeba watu 60.

• Wapi ambapo ukimsindikiza mtu eapot, anaweza akafika South Afrika wakati wewe bado uko kwenye foleni hujafika kwenu?

No comments:

Post a Comment