May 27, 2014

Profesa Mark Mwandosya ziarani Burundi

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya na Mkewe mama Lucy Mwandosya wakitoa heshima kwenye kaburi la Louis Rwagasore aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Burundi aliyeuawa Oktoba 1961
Waziri Mwandosya akutana na maafisa kutoka kiwanda cha saruji cha Mbeya Cement na mawakala wa Mbeya Cement Burundi.Waziri Mwandosya aliwapongeza Mbeya Cement kwa kuwa wauzaji wakubwa wa saruji Burundi.Aliwahimiza kuongeza juhudi kupanua soko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kutoka kushoto ni Ephraim Kalinga,Meneja wa Mauzo ya nje Mbeya Cement,Waziri Mwandosya,Emil Sindato ,Meneja Ufundi Mbeya Cement, Debrah Hernandez,mwakilishi wa wakala,na Eric Aneca,mwalikilishi wa wakaala wa Mbeya Cement.

No comments:

Post a Comment