May 28, 2014

MTAALA KUBADILISHWA KUPUNGUZA MIMBA ZA UTOTONI



MTAALA KUBADILISHWA KUPUNGUZA MIMBA ZA UTOTONI

Serikali inatarajia kuweka katika mtaala wa elimu unaotumika sasa, somo la afya ya uzazi kwa vijana katika shule za msingi na sekondari nchini kupunguza mimba za utotoni na maambukizi ya Ukimwi.Hayo yalisemwa jana, Dar esSalaam na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Jenista Mhagama katika ufunguzi wa mkutano wa siku tatu kuhusu 
afya ya uzazi kwa vijana uliozishirikisha nchi 16.Mhagama alisema 
serikali imeweka mikakati ya kuanzisha elimu hiyo ya afyaya uzazi na 
jinsia kwa vijanakatika shule za msingi kutokana na ukubwa wa tatizo 
la mimba za utotoni namaambukizi ya Ukimwi."Serikali inawahakikishia 
wanasayansi kuwa elimu hiyo itawapa matokeo chanya kwamba hakutakuwa 
na maambukizi wala mimba za utotoni kwa vijana hao,'' alisema Mhagama 
katika hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi Msaidizi wa 
masuala mtambuka katika wizara hiyo, Letisia Sayi.Mhagama alisema 
elimu ya afya ya uzazi kwa vijana itasaidia kubadili tabia, kujikinga 
kwa kutumia kondomu na wanaoishi na maambukizi kulinda afya zao.Naye, 
Mtaalamu wa kitaifa wa masuala ya Ukimwi na elimu ya afya wa Shirika 
la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Martin Herman alisema takwimu 
za wizara hiyo zinaonesha wanafunzi 6000 kila mwaka wanaacha shule kwa 
sababu ya mimba za utotoni.Herman alisema mpango huo wa kutoa elimu ya 
afya utaanza Julai mwaka huu baada ya mapitio ya mtaala huo na 
inatarajiwa ifikapo mwaka 2015 wanafunzi watajua afya ya uzazi na 
kupata walimu waliobobea katika masomo hayo.Nchi zilizoshiriki mkutano 
huo ni pamoja na Afrika Kusini, Kenya, Sweden, Uganda, Malawi, 
Zimbabwe, Zambia, Burundi, Namibia, Rwanda, Botswana, 
Lesotho,Swaziland, Angola, Ethiopia na wenyeji Tanzania


No comments:

Post a Comment