May 20, 2014

JB ADONDOKA AKIMUELEZEA MAREHEMU KUAMBIANA

 
 
 
 
Msanii Jacob Steven 'JB' amedondoka katika Viwanja vya Leaders wakati akimuelezea msanii mwenzake marehemu Adam Kuambiana. Tukio hilo limetokea wakati wa zoezi la kuaga mwili wa marehemu kabla ya maziko yatakayofanyika baadaye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Marehemu Kuambiana alifariki dunia ghafla Jumamosi ya Mei 17 mwaka huu wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar.




No comments:

Post a Comment