May 19, 2014

Fahamu umaarufu wa Ngorongoro Crater kwa kusoma hapa



DSC_0813
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
DSC_0012
Na Mwandishi wetu
Ngorongoro Crater ni miongoni mwa maajabu saba ya dunia ukiwamo Mlima Kilimanjaro. Ni mwendo wa sana Tumbili na Nyani aina mbalimbali. Na usipokuwa mwangalifu na kuacha milango na madirisha wazi Soda, Biskuti na Ndizi mbivu ulizochukua kwa kujikimu na njaa ya siku nzima ukiwa mbugani, utakuta hakuna hata nyaraka.   Kama watazisoma au hapana hilo si jukumu lako ila utakuwa umepoteza nyaraka muhimu.
Ngorongoro Crater ni mbuga za wanyama mfano wa bakuli kubwa lililoundwa miaka 25 elfu iliyopita baada ya milima miwili Makaroti na Satiman kulipuka na kutoa tope lenye moto. Tope hili ndilo lilikuwa na tabaka tatu za udongo na kuumba bonde lililofanana na bakuli kubwa ambalo wenyeji wa kabila la Kimasai walilipa jina la Ngorongoro Kaldera.
DSC_0854
Kijiji cha Malanja ni cha pekee katika bonde la Ngorongoro katikati ya Milima ya Makaroti ambao ni mkubwa na Satiman ambao ni mdogo. Wenyeji wa kijiji hicho huendesha Maisha yao kama kawaida ya kufuga mifugo yao ndani ya mbuga wakichanganyika na wanyama pori.
DSC_0862
Katika bonde hilo kuna mto mmoja ambao unatoka Olmot Crater, Ziwa Magadi ambalo wakati wa kiangazi hukauka na kutoa vumbi aina ya majivu ambayo wenyeji wa Kimasai hutumia kuwalisha Ng’ombe kama dawa ya kudhibiti magonjwa.
DSC_0909
Huwezi kuzungumzia hifadhi ya Ngorongoro Crater bila kuwataja wanyama wakubwa wajulikanao kama “Big Five”, ambao ni Faru, Tembo, Chui, Nyati na Simba. Lakini kwa mujibu wa kiongozi wa msafara wa utalii, Kwa sasa kuna Big Six akiwemo Mmasai kwa kile kinachoitwa kuwa karibu na mbuga hiyo na kuishi na wanyama bila kudhuriana.
DSC_0981
Twiga pamoja na kwamba anatajwa kuwa miongoni mwa wanyama wanaotajwa kuwemo katika hifadhi, lakini yeye hakai katika bonde kutokana na mazingira ya malisho yake- hakuna miti mirefu na kutokana na shingo yake kuwa ndefu hawezi wakati wote kuinama kutafuta malisho lakini pia aina ya majani ambayo mnyama huyo hupendelea kula nakakosekana katika bonde la Ngorongoro.
Swala au Mbuzi pori kama ajulikanavyo na wengi, pia hayuko katika bonde hilo kutokana na ukweli kwamba yeye hupenda kuishi katika vichana jambo ambalo haliko katika bonde hilo.
DSC_0828
Wanyama wengi hupata maji katika mto mmoja tu uliopo katika bonde la Ngorongoro ujilikanao kama Munge.
Nyumbu ni mnyama mwenye sifa ya pekee, kwanza ndio walio wengi katika mbuga, wapole, wanaonewa sana na wanyama wanaokula nyama lakini kikubwa ni kwamba mtoto wa Nyumbu akizaliwa, ana uwezo wa kukimbia kwa spidi ya mama yake ndani ya dakika 10.
DSC_0975
Kinachovutia zaidi ni kuona wanyama wote, wakali na wapole jinsi wanavyoishi kwa pamoja hadi pale tu wanapokuwa na njaa ndio hubadilikianana. Penye kundi la Nyumbu, Faru, Punda milia, Ngiri, Nguruwe na kadhalika utawakuta pia Simba pembeni wamelala wakipunga upepo baada ya kupata mlo wa mchana. Hii ni kuonyesha kwa jinsi gani wanaishi kama familia moja na wako katika nyumba moja.
DSC_1006
DSC_0960
Tofauti iko kwa Nyati. Mara nyingi mnyama huyu huwa hana urafiki na wanyama wengine wanaokula majani kama wao. Mara nyingi utawakuta wao wako kwa umbali mdogo kutoka walipo wanyama wengine.
DSC_0844
DSC_0948
Siku za utoto wangu nilikuwa nikiamini kuwa ndege mkubwa ambaye huruka ni Tai. Lakini kwa maajabu ya Ngorongoro yuko ndege mkubwa na mzito ambaye huruka kama tai.
DSC_1054
Hifadhi ya Ngorongoro yenye ukubwa wa kilometa 210 inastahili sifa zote za kuwa miongoni mwa maajabu saba duniani. Ni mahali ambapo mbali ya kuona wanyama mbalimbali hususan faru weusi ambao huogopewa kwa ukali, Tembo wakubwa wazee na ndege aina ya ‘Flamingo’, pia  kuna hali ya hewa ya pekee ambayo inavutia kuishi hasa kwa watu wasiopenda mazingira ya joto kali.
DSC_0904
DSC_0914
Wadau wa sekta ya Habari nchini wakiwa katika Hifadhi ya Ngorongoro.
DSC_0021
Picha juu na chini Baadhi ya wadau wa sekta ya Habari waliopata nafasi ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani iliyofanyika jijini Arusha hivi karibuni.
DSC_0745

No comments:

Post a Comment