February 24, 2015
Chadema yaigaragaza vibaya CCM uchaguzi wa serikali za mitaa Sumbawanga mkoani Rukwa...Chadema yanyakua mitaa 37 CCM yaambulia mitaa 5
Wafuasi wa Chadema wakishangilia katika Kata ya Chanji baada ya chama hicho kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa marudio wa Serikali za Mitaa uliofanyika juzi mjini Sumbawanga.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeigaragaza vibaya CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika juzi katika kata tatu za Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ambazo hazikufanya uchaguzi Desemba 14, mwaka jana.
Uchaguzi katika kata hizo uliahirishwa kutokana na kasoro mbalimbali jambo lililosababisha mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, William Shimwela kusimamishwa kazi.
Msimamizi wa uchaguzi huo uliofanyika katika kata za Msua, Chanji na Kizwite na mitaa mingine miwili iliyorudia uchaguzi, Hamid Njovu alisema Chadema ilinyakua jumla ya mitaa 37 kati ya 44 na kuiacha CCM ikiambulia mitaa mitano.
Matokeo hayo mapya yanaibuka sasa wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilishahitimisha kutangaza matokeo ya jumla ya mitaa katika uchaguzi huo ikisema ulikuwa umekamilika kwa asilimia 100.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tamisemi, Kalist Luanda alisema Desemba 24, mwaka jana kuwa mitaa yote 3,875 nchini ilifanya uchaguzi na kukamilika kwa asilimia 100 huku CCM ikipata asilimia 66.66 baada ya kuzoa mitaa 2,583, ikifuatiwa na Chadema iliyopata mitaa 980 (asilimia 25.3), CUF mitaa 266 (asilimia 6.9), NCCR Mageuzi mitaa 28 (asilimia 0.7), TLP mtaa mmoja (asilimia 0.03), ACT mitaa 12 (asilimia 0.31), UDP mitaa mitatu (asilimia 0.08), NRA mtaa mmoja (asilimia 0.03) na UMD mtaa mmoja (asilimia 0.03).
Matokeo mapya
Akitangaza matokeo hayo jana, Njovu alisema katika Kata ya Kizwite kati ya mitaa 15 iliyofanya uchaguzi Chadema ilishinda mitaa 13 dhidi ya CCM iliyoambulia mitaa miwili, Kata ya Msua mitaa yote 13 iliyofanya uchaguzi ilikwenda kwa Chadema na CCM kuambulia patupu.
Alisema kwa Kata ya Chanji ambayo ilikuwa na mitaa 14 iliyofanya uchaguzi, Chadema ilishinda mitaa 10 na CCM mitatu huku mtaa mmoja wa Nankasi kura ziligongana katika nafasi ya uenyekiti, hivyo kuamuliwa uchaguzi utarudiwa Jumapili.
Njovu alisema katika uchaguzi wa marudio uliofanyika kwenye mitaa miwili kila chama, CCM na Chadema, kiliibuka na ushindi katika mtaa mmoja ambao mtaa wa Bangwe Kata ya Izia ulichukuliwa na CCM na ule wa Tambazi katika Kata ya Sumbawanga ukaenda Chadema.
Uchaguzi huo uliofanyika kwa amani na utulivu tofauti na ilivyokuwa Desemba 14, mwaka jana ambapo ulivurugika katika kata hizo kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza ikiwa pamoja na vituo kuchelewa kufunguliwa.
Hali hiyo ilisababisha wananchi waliokaa vituo kwa zaidi ya saa nane wakisubiri kupiga kura kuhamaki na kujichukulia sheria mkononi kwa kuchoma moto ofisi ya mtendaji wa kata ya Kizwite na Chanji na kuteketeza nyaraka zote za kupigia kura, hivyo kufanya mchakato mzima wa uchaguzi huo kufanyika upya.
Akizungumza baada ya matokeo hayo, Mwenyekiti wa Chadema mkoani Rukwa, Zeno Nkoswe aliwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wingi kupiga kura na kufanya Chadema kuibuka na ushindi wa kimbunga na kuwa huo ni mwanzo wa kuelekea ukombozi wa Taifa kutoka mikononi mwa CCM.
Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Rukwa, Clement Bakuli alisema wameyapokea matokeo hayo kwa masikitiko, lakini katika mpambano wowote lazima mshindi apatikane, hivyo chama kitakaa kufanya tathmini kuona wamekosea eneo gani ili waweze kujirekebisha katika uchaguzi ujao.
Pamoja na matokeo hayo, timu nzima ya CCM ngazi ya wilaya ikiongozwa na mwenyekiti wake wa mkoa, Emmanuel Kilindu na Mbunge wa Sumbawanga Mjini Aeshi Hilaly walipiga kambi na kufanya kampeni za nguvu katika kata hizo lakini haikufua dafu.
Ushindi huo ni mwendelezo wa mafanikio ya Chadema ndani ya Ukawa katika uchaguzi huo Desemba 14 na kurudiwa Desemba 21 katika baadhi ya maeneo, yaliyoonyesha kuwa uungwaji mkono wa CCM katika maeneo ya mijini umeporomoka kwa kasi huku wa upinzani ukiimarika.
Katika uchaguzi huo, chama kipya cha ACT-Tanzania kilichomoza na kuviacha baadhi ya vyama vikongwe ambavyo havikupata hata nafasi ya ujumbe katika uchaguzi ulioelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) kuwa ulikuwa umekamilika kwa asilimia 99.
Katika maeneo ya vijiji na vitongoji, CCM ilipata ushindi wa asilimia 79.81 (vijiji) na 79.83 katika vitongoji, wakati kwenye mitaa ambayo ipo sehemu za mijini kilishuka zaidi na kupata asilimia 66.66, ikilinganishwa na matokeo ya uchaguzi wa mwaka 1999, ambapo chama hicho kilipata asilimia 89.2 katika mitaa, asilimia 91 katika vitongoji na asilimia 91.6
MKURUGENZI ALEX MSAMA AMWAGA MISAADA KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA, ALAANI MAUAJI YA ALBINO YANAYOENDELEA NCHINI
Alex Msama amelaani mauaji ya Albino na kuiomba serikali kuweka mkazo katika kushughulikia wahalifu wanaofanya ukatili huu na kuua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), ili kukomesha mauaji hayo hapa nchini ambayo yanalitia aibu taifa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Honorata Michael Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Honorata kilichopo Temeke jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Rashid Mpinda Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni Mosco jijini Dar es Sakaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Soud Said Mwakilishi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Ijanzo Zanda orphanage Centre cha jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Hadija Mwambungu kutoka kituo cha kulelea watoto yatima cha Malaika Kids kilichopo Mwananyamala Mwinjuma jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akiakihelezea zaidi kwa waandishi wa habari juu ya misaada hiyo iliyotolewa na kampuni yake kwa vituo hivyo wakati huu wa maandalizi ya tamasha la Pasaka.
Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Bw Hudson Kamoga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha la pasaka.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akiakiwa amewabeba baadhi ya watoto wa kituo cha Honorata wakati alipowakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akihojiwa na mwaandishi wa habari wa BBC Bw. Anold Kayanda mara baada ya kukabidhi misaana hiyo ambapo aliiomba serikali kuweka mkazo katika kushughulikia wahalifu wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)ili kukomesha mauaji hayo hapa nchini
February 19, 2015
MORE NATURAL GAS DISCOVERED IN TANZANIA LIVE STORY!!
The new gas discovery was made in the same Lower Cretaceous sandstones as the gas discovery in the Zafarani-1 well drilled in 2012.
Dar es Salaam. Statoil is upbeat on the discovery of natural gas offshore Tanzania.
The discovery of an additional 2 trillion to 3 trillion cubic feet (tcf) of natural gas in the Piri-1 well brings the total of in-place volumes up to about 20 tcf in Block 2. "Since 2012 we have had a 100 per cent success rate in Tanzania and the area has become a core exploration area in a very short period of time," said Mr Nick Maden, senior vice president for Statoil's exploration activities in the Western Hemisphere, in a statement yesterday.
"We quickly went from drilling one well to a multi-well programme and with Piri-1 we are continuing the success." The new gas discovery was made in the same Lower Cretaceous sandstones as the gas discovery in the Zafarani-1 well drilled in 2012.
The discovery is Statoil and co-venturer ExxonMobil's sixth and the fifth high impact discovery in Block 2 offshore Tanzania. It was preceded by the four successful high-impact gas discoveries, Zafarani-1, Lavani-1, Tangawizi-1 and Mronge-1, and a sixth discovery in the Lavani-2 well beneath the Lavani-1 discovery. "Additional prospectivity has been mapped and will be tested throughout 2014 and 2015. We expect to drill several additional exploration and appraisal wells and hope that the results from these wells will continue to add gas volumes for a future large-scale gas infrastructure development," said Maden.
Statoil operates the licence on Block 2 on behalf of Tanzania Petroleum Development Corporation and has a 65 per cent working interest. ExxonMobil Exploration and Production Tanzania Limited hold the remaining 35 per cent. Tanzania is a growing market with ongoing exciting discoveries, including 19 exploration blocks and $10-20 billion investment projected for exploration and production in the coming decade. Over the past two years, exploration in Tanzania's deep offshore waters have led to the discovery of about 45 tcf of gas.
February 15, 2015
BREAKING NEWS: MOTO WATEKETEZA NYUMBA MAENEO YA UBUNGO KIBANGU

HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE MOTO MKUBWA UMEZUKA KATIKA NYUMBA ILIYOKO MAENEO YA UBUNGO KIBANGU NA KUSABABISHA TAFRANI KUBWA MAENEO HAYO... MALI BADO ZINAENDELEA KUOKOLEWA HUKU KUKIWA NA UTEKETEAJI WA MALI NYINGI ZAIDI KWA MOTO HUO,,,WANANCHI WANAENDELEA NA UOKOAJI...CHANZO CHA MOTO HUO BADO HAUJAFAHAMIKA.....
February 14, 2015
VIDEO: Majigambo ya Vijana wa Tanga (Magaidi) Baada ya kuwapora Silaha Polisi
Matokeo ya Kidato cha NNE 2014
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
CSEE 2014 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES
DISTINCTION | MERIT | CREDIT | PASS | FAIL | |
GPA | 3.6 - 5.0 | 2.6 - 3.5 | 1.6 - 2.5 | 0.3 - 1.5 | 0.0 - 0.2 |