May 18, 2014

WENGER ASEMA KUBEBA KOMBE LA FA HAKUMBAKIZI ARSENAL

 

Shower time: Lukas Podolski of pours beer over Wenger after their FA Cup win

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ushindi dhidi ya Hull City na kunyakua kombe la FA hakuchangii chochote katika maamuzi yake ya kuendelea kubaki Emirates.

Baada ya mechi hiyo iliyomaliza kiu ya miaka 9 ya ukame wa mataji, Wenger alithibitisha rasmi kuwa haondoki Arsenal, lakini akasisitiza kuwa matokeo ya mechi hiyo iliyopigwa uwanja wa Wembley hayahusiani na maamuzi yake hayo.

Going nowhere: Arsenal boss Arsene Wenger has confirmed he will be staying on as manager

"Siku zote nimekuwa nikisema hatma yangu haihusiani na mechi hii, lakini mara zote nimekuwa nikitaka kubaki Arsenal," Wenger aliiambia ITV pale alipoulizwa kama anabaki, kabla hajasema, "Ndiyo, nitabaki."

No comments:

Post a Comment