May 24, 2014

RONALDO KAMILI GADO KUWASASAMBUA ATLETICO MADRID FAINALI YA UEFA



RONALDO KAMILI GADO KUWASASAMBUA ATLETICO MADRID FAINALI YA UEFA

Thumbs up: Cristiano              Ronaldo is expected to be fit for Real Madrid's Champions              League final showdown

No problems: Ronaldo                    trained well during Friday's practice session                    according to manager Carlo Ancelotti
Big match: Ronaldo and                        his team-mates are looking to land Real Madrid's                        10th European Cup triumph
Big match:                        Ronaldo and his team-mates are looking to land                        Real Madrid's 10th European Cup triumph
 Imechapishwa Mei 23, 2014, saa 11: 15 usiku
MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo anatarajia kuiongoza Real Madrid katika mchezo wa fainali ya UEFA kesho jumamosi dhidi ya mahasimu wao wa jiji, Atletico Madrid, amesema kocha Carlo Ancelotti.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno hajacheza tangu alipopata majeruhi katika sare ya 1-1 dhidi ya Valladolid mei 7 mwaka huu, na alitarajiwa kucheza katika mechi ya mwisho ya La Liga dhidi ya Espanyol, lakini aliondolewa katika kikosi ikiwa ni tahadhari ya mchezo wa kesho wa UEFA.
Hata hivyo katika mazoezi ya leo mjini Lisbon, Ronaldo ameonekana kama hana tatizo lolote, hivyo kesho atapambana kutafuta ubingwa wa 10 wa UEFA kwa Real Madrid.
'Mazoezi ya leo ni muhimu sana. Nadhani Ronaldo hana tatizo lolote". Alisema Ancelotti katika mkutano na waandishi wa habari leo ijumaa.


No comments:

Post a Comment