May 15, 2014

LIVERPOOL YAZINDUA UZI WAO MPYA WA UGENINI …Suarez asema bado yupo yupo sana

 
 
 
 

Keeping it cool: Reds stopper Simon Mignolet (right) shows off the black away keeper's kit

LIVERPOOL wametambulisha jezi zao mpya za ugenini kwa msimu ujao huku nyota wao Luis Suarez akionyesha nia ya kubaki Anfield.

Safari hii Liverpool wamekwenda kwa rangi ya njano, hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2007.

Key men: Daniel Sturridge, Luis Suarez and Steven Gerrard helped unveil the Liverpool away kit for 2014/15

Wekundu hao ambao wameukosa ubingwa wa England kwa ncha, tayari wameanza kuangalia kampeni za msimu ujao.

Mshambuliaji Luis Suarez alikuwa miongoni mwa wachezaji waliopozi kwa picha za jezi mpya, hali inayodhihirisha kuwa nyota huyo hana mpango wa kuchomoka Liverpool.

Suarez akasema: "Akili yangu kwa sasa ipo kwenye Kombe la Dunia. Najua nitatawala vyombo vya habari kwenye tetesi za usajili, lakini mimi nina mkataba na Liverpool na nina furaha kuwa hapa."

No comments:

Post a Comment